Tanga Cement
Terms of Use   |   Sitemap   |   Privacy   |   Contacts   |   FAQs   |  
 Home |  Our Company |  Products & Services |  Investor Relations |  Sustainable Development |  People & Jobs |  Media Centre |
Media Centre
  News
  Media Releases
  TCCL in the Press
  Archives
  About Tanga
Home : Media Centre : News
 
Media Release:

Taarifa kuhusu mradi wa upandaji miti eneo la kiwanda cha saruji  - tanga.

 

Tanga, 06 July 2012

UTANGULIZI
Taarifa hii imeandaliwa kwa ajili ya mbio za Mwenge wa Uhuru katika wilaya ya Tanga siku ya tarehe 6/7/2012, ikiwa ni pamoja na uwekaji jiwe la uzinduzi wa mradi wa upandaji miti pembezoni mwa eneo la kiwanda.

 HISTORIA
Mradi wa upandaji miti eneo la kiwanda cha Tanga Cement ulianzishwa mwaka 2010,katika eneo lililokuwa la majaribio ya miti aina ya Jatrofa. Miti ya Jatrofa ilitegemewa kutoa nishati mmbadala, lakini mradi haukufanikiwa, hivyo kampuni ikaamua eneo hilo lipandwe miti  aina ya mitiki.

Awamu ya kwanza , ya upandaji miti ilihusisha eneo la hecta 25, sawa na eka 56, zikiwa zi megawanywa kwenye ploti 4, na kupandwa miti 3600 kati ya mwezi October 2010 na Januari 2011. Miche ya mitiki  ilipatikana kutoka shamba la Miche katika msitu wa Longuza huko Muheza, na kutoka vitalu binafsi jijini Tanga. Hadi leo hii miti iliyopandwa awamu ya kwanza mingi  imeshafikia urefu wa mita 3 na zaidi.
Awamu ya pili ambayo imeanza mwanzoni mwaka huu 2012 imehusisha eneo la hekta 6, sawa na ekari 15 ambalo limepandwa miti aina ya Mikaratusi, kiasi cha miti 9,200, lengo likiwa kufikisha miti 10,000 ifikapo mwishoni mwa mwezi Julai mwaka huu.  Miche ya mikaratusi tumeipata kutoka mradi wa Taifa wa miti kule Korogwe -maili kumi, katika kituo cha miche cha TAFORI ambao wametoa wataalamu na ushauri kuhusu upandaji.

Tunategemea pia  kuwa na awamu ya tatu ya mradi  katika eneo lililobakia la ukubwa wa hecta 16, na awamu hii tunayotegemea kuianza mwakani, nayo pia  tutapanda mikaratusi au aina nyingine kama wataalamu  wa misitu watakavyotushauri. Mradi wa upandaji miti utakuwa endelevu, ukiendelezwa kwa awamu katika maeneo ya wazi ambayo tunayamiliki kisheria.

SABABU NA FAIDA ZA KUANZISHA MRADI

 • Eneo lililopandwa miti lilikuwa eneo la wazi kati ya kiwanda na barabara ya Tanga  - Korogwe ambalo tumelihifadhi kwa ajili ya mali ghafi ya baadaye  (Udongo wa mfinyanzi) kwa matumizi ya uzalishaji (Future mining area).
 • Eneo hili kubaki wazi linashawishi uvamizi ( enchroachement), hivyo tukaamua litumike  kwa upandaji miti wakati tunasubiri uchimbaji udongo huko mbeleni.
 • Eneo la miti linakuwa buffer zone ,kati ya kiwanda  na makazi.
 • Miti itasaidia kuchuja vumbi na hewa ukaa kutoka kiwandani, kwani hewa ukaa (CO2) ndiyo chakula cha miti, na viwanda vya Saruji hutoa hewa ukaa nyingi. .
 • Miti hupendeza manthari ya eneo (Environmental aesthetics).
 • Tunampango wa kutumia mradi huu kuombea “Carbon credits” ambayo itakuwa faida kwa kampuni  na kurejesha sehemu ya gharama.
 • Miti hii inaweza kutumika kama nishati  mmbadala kiwandani ili kupunguza wingi wa nishati ya mafuta na mkaa wa mawe na hivyo kuendeleza kulinda mazingira.
 • Inaweza kutumika kwa ajili ya mbao hivyo kuwa faida kwa kiwanda.
 • Miti pia itazuia mmonyokoko wa udongo na kulinda/kuongeza rutuba kwenye ardhi.
 • Mradi huu umetoa ajira ya muda kwa vijana wakati wa upandaji na unaendelea kutoa ajira wakati wa utunzaji.

KWANINI MITIKI NA MIKARATUSI?

 • Mitiki inahimili moto , utunzaji  wake ni rahisi, lakini pia inafaida  kama nguzo, mbao , inatunza mazingira na ikivunwa huchipua tena.
 • Kwa upande wa  mikaratusi kuna dhana kwamba hukausha maji ardhini, lakini tumehakikishiwa na wataaalam kwamba jamii ya mikaratusi tuliyopanda, kati ya jamii (species) mia sita za mikaratusi,  mahitaji yake ya maji ni kidogo, na inafaa katika maeneo ya ukame kiasi.
 •  Ndege pia hupenda kujenga viota kwenye miti hii kwani inakuwa mirefu ,hivyo kuwahakikishia usalama wa viota vyao.
 •  Inafaa kwa nguzo za umeme na simu kwani haipekechwi  wala kudhuriwa na mchwa.

GHARAMA ZA MRADI
Awamu ya kwanza, iligharimu jumla ya Tsh 20M (Milioni ishiririni)

 • Awamu ya pili inayoendelea sasa hivi imegharimu Tsh. 22M (milioni ishirini  na mbili), ikiwa ni pamoja na utunzaji hadi mwishoni mwa mwaka huu. Pamoja na kwamba eneo hili ni dogo lakini limepandwa miti mingi ukilinganisha na lilopandwa mitiki – mikaratusi ni 10,000 na Mitiki ni 3600.
 • Mradi huu umegharamiwa na Kampuni ya Tanga cementi, kama mfadhili pekee.

MENGINEYO:  Kampuni pia imepanda miti 2600  kuzunguka mipaka yake yote. Na pia imepanda miti ya asili kwenye machimbo yaliyohamwa na  kulirudisha eneo hilo kuwa kwenye mazingira ya awali.

HITIMISHO:
Tunashukuru uongozi wa Mkoa na Wilaya kuutambua mradi huu na kuuweka katika ratiba ya mwenge , kwani kuutangaza hivi ni njia mojawapo ya kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa upandaji miti. Hii pia imelenga sera ya  kampuni kuhusu  mazingira (TCCL Environment Policy) ambayo kipengele kimoja wapo kinalenga kushirikisha  na kuhamasisha jamii na wadau kuhusu  utunzaji  wa mazingira.

 

 
   
   
   
   
   
   

 

 
News Room
  News Headlines
  Media Releases